فَلَمَّا رَءَآ أَيۡدِيَهُمۡ لَا تَصِلُ إِلَيۡهِ نَكِرَهُمۡ وَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۚ قَالُواْ لَا تَخَفۡ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمِ لُوطٖ ٧٠
Falammā ra'ā aydiyahum lā tasilu ilayhi nakirahum wa awjasa minhum khīfatan qālū lā takhaf innā ursilnā ilā qawmi lūt
Basi alipoona mikono yao haimfikilii aliwatilia shaka, na akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut'. 70
Maelezo ya chini
70 Alipoona kuwa hawanyooshi mikono yao kama ada ya wageni akawatilia shaka kuwa hawa si wageni wa kawaida, na akahisi kuwa hawa ni Malaika. Ikamjia khofu kuwa isije kuwa kuja kwao ni kwa jambo ambalo halikumpendeza Mwenyezi Mungu, au kuwaadhibu watu wake. Wakasema, nao walijua athari ya ile khofu katika nafsi yake: Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kuwahiliki kaumu Lut'.