Surat Az-Zukhruf, aya 58

43:58

وَقَالُوٓاْ ءَأَٰلِهَتُنَا خَيۡرٌ أَمۡ هُوَۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلَۢاۚ بَلۡ هُمۡ قَوۡمٌ خَصِمُونَ ٥٨

Waqālū a'ālihatunā khayrun am huwa mā darabūhu laka illā jadalā bal hum qawmun khasimūn

Wakasema: Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu? Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi! 58

Maelezo ya chini

58 Makafiri wamesema: Je! Miungu yetu na Isa, nani bora? Ikiwa yeye yuko Motoni basi sisi na miungu yetu tutakuwa pamoja naye. Hawakupigii mfano huu wewe ila kutafuta ubishi tu, na kushindana kwa maneno, si kwa ajili ya kuitafuta kweli ilivyo. Bali hawa ni watu ambao ni shadidi wa khasama, wamebobea kwa hayo.