Surat At-Tawbah, aya 115

9:115

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِلَّ قَوۡمَۢا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰهُمۡ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٌ ١١٥

Wamā kānallāhu liyudilla qawmā ba'da idh hadāhum hattā yubayyina lahum mā yattaqūna innallāha bikulli shay'in 'alīm

Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwahisabu watu kuwa wamepotea baada ya kwisha waongoza mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. 115

Maelezo ya chini

115 Na si katika mwendo wa Mwenyezi Mungu na upole wake kwa waja wake kuwachukulia watu kuwa wamepotea, na awapitishie hukumu ya kuwatia khatiani na kuwapa adhabu, baada ya kwisha waongoza njia ya Uislamu, mpaka awabainishie kwa njia ya wahyi, ufunuo, kwa Mtume wake mambo ambayo inawapasa wajiepushe nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu.