إِنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۚ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٖ ١١٦
Innallāha lahū mulkus-samāwāti wal-ardi yuhyī wayumītu wamā lakum min dūnillāhi min waliyyin walā nasīr
Hakika Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi; huhuisha na hufisha. Nanyi hamna Mlinzi wala Msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu. 116
Maelezo ya chini
116 Hakika ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mmiliki wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na Yeye ndiye Mwenye kuvisarifu viliomo humo kwa uhai na mauti. Na nyinyi hamna ila Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa kutawala mambo yenu, wala hamna Msaidizi mwingine wa kukunusuruni na kukulindeni.