Surat At-Tawbah, aya 114

9:114

وَمَا كَانَ ٱسۡتِغۡفَارُ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوۡعِدَةٖ وَعَدَهَآ إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥٓ أَنَّهُۥ عَدُوّٞ لِّلَّهِ تَبَرَّأَ مِنۡهُۚ إِنَّ إِبۡرَٰهِيمَ لَأَوَّٰهٌ حَلِيمٞ ١١٤

Wamā kānastighfāru ibrāhīma li abīhi illā 'am maw'idatin wa'adahā iyyāhu falammā tabayyana lahū annahū 'aduwwu lillāhi tabarra'a minhu inna ibrāhīma la awwāhun halīm

Wala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake ila kwa sababu wa ahadi aliyo fanya naye. Lakini ilipo mbainikia kwamba yeye ni adui ya Mwenyezi Mungu, alijiepusha naye. Hakika Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba, mnyenyekevu, mvumilivu. 114

Maelezo ya chini

114 Haikuwa vile alivyo fanya Ibrahim a.s. kumtakia msamaha baba yake ila ni kutimiza ahadi aliyo ahidi Ibrahim kumuahidi baba yake, kwa kutaraji kuwa atakuja amini. Ilipo kwisha mbainikia Ibrahim kuwa huyo ni adui wa Mwenyezi Mungu kwa kushikilia kwake ushirikina mpaka akafa na ukafiri, Ibrahim alijitenga naye, na akaacha kumwombea maghfira. Na Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba, na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, na mstahamilivu kwa maudhi.