فَمَآ أُوتِيتُم مِّن شَيۡءٖ فَمَتَٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ ٣٦
Famā ūtītum min shay'in famatā'ul-hayawātid-dunyā wamā 'indallāhi khayrun wa abqā lilladhīna āmanū wa'alā rabbihim yatawakkalūn
Basi vyote mlivyo pewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora, na cha kudumu kwa ajili ya walio amini, na wakawa wanamtegemea Mola wao Mlezi, 36
Maelezo ya chini
36 Msidanganyike na starehe za dunia. Kwani enyi watu! Yote mliyo pewa, mali, wana, na vyenginevyo, ni starehe zenu za maisha ya duniani. Na aliyo yaandaa Mwenyezi Mungu katika neema za Peponi ni bora na zinadumu zaidi kwa wenye kuamini, na kumtegemea Muumba wao na Mlezi wao wa pekee;