Surat Ash-Shura, aya 18

42:18

يَسۡتَعۡجِلُ بِهَا ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِهَاۖ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مُشۡفِقُونَ مِنۡهَا وَيَعۡلَمُونَ أَنَّهَا ٱلۡحَقُّۗ أَلَآ إِنَّ ٱلَّذِينَ يُمَارُونَ فِي ٱلسَّاعَةِ لَفِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٍ ١٨

Yasta'jilu bihal-ladhīna lā yu'minūna bihā walladhīna āmanū mushfiqūna minhā waya'lamūna annahal-haqqu alā innal-ladhīna yumārūna fis-sā'ati lafī dalāli ba'īd

Wasio amini huihimiza hiyo Saa ifike upesi; lakini wanao amini wanaiogopa, na wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ama kwa hakika hao wanao bishana katika khabari za hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa. 18

Maelezo ya chini

18 Wanahimiza ije Saa ya Kiyama upesi upesi, kwa maskhara, hao wasio iamini. Na wenye kuiamini wamo katika khofu isitokee. Hao hawaihimizi. Na wanajua kuwa hiyo ni kweli iliyo thibiti, wala haina shaka. Naye Subhanahu anazindua kwamba hao wanao bisha kuja kwake bila ya shaka wamo katika upotovu ulio mbali na Haki.