Surat An-Nisa, aya 154

4:154

وَرَفَعۡنَا فَوۡقَهُمُ ٱلطُّورَ بِمِيثَٰقِهِمۡ وَقُلۡنَا لَهُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُلۡنَا لَهُمۡ لَا تَعۡدُواْ فِي ٱلسَّبۡتِ وَأَخَذۡنَا مِنۡهُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا ١٥٤

Warafa'nā fawqahumut-tūra bimīthāqihim waqulnā lahumudkhulul-bāba sujjadan waqulnā lahum lā ta'dū fis-sabti wa akhadhnā minhum mīthāqan ghalīzā

Na tukanyanyua mlima juu yao kwa kufanya agano nao. Na tukawaambia: Ingilieni mlangoni kwa unyenyekevu. Na tukawaambia: Msiivunje Siku ya Sabato (Jumaa mosi). Na tukachukua kwao ahadi iliyo madhubuti. 154

Maelezo ya chini

154 Mwenyezi Mungu akaunyanyua mlima juu ya Wana wa Israili ili kuwatisha kwa kule kuikataa kwao sharia ya Taurati, mpaka wakaikubali. Akachukua kwao agano, na akawaamrisha waingie mjini hali wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Wala wasiyakiuke aliyo waamrisha kushika ibada katika siku ya Sabato, yaani Jumaamosi.(Imeitwa "Sabt" Kiarabu, "Shabbath" Kiyahudi, "Sabbath" Kiingereza, na "Sabato" Kiswahili, maana yake "Mapumziko" kwa kuwa ni siku ya mapumziko kwa Mayahudi.) Na Mwenyezi Mungu alichukua kwao ahadi ya nguvu.