فَبِمَا نَقۡضِهِم مِّيثَٰقَهُمۡ وَكُفۡرِهِم بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَقَتۡلِهِمُ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَقَوۡلِهِمۡ قُلُوبُنَا غُلۡفُۢۚ بَلۡ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَيۡهَا بِكُفۡرِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُونَ إِلَّا قَلِيلٗا ١٥٥
Fabimā naqdihim mīthāqahum wakufrihim bi'āyātillāhi waqatlihimul-ambiyā'a bighayri haqqin waqawlihim qulūbunā ghulfu bal taba'allāhu 'alayhā bikufrihim falā yu'minūna illā qalīlā
Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi zao, na kuzikataa kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri kwa kufuru zao, basi hawaamini ila kidogo tu. 155
Maelezo ya chini
155 Mwenyezi Mungu akawakasirikia kwa sababu ya kuvunja agano hili, na kuzikataa ishara za Mwenyezi Mungu, na kwa kuwauwa Manabii kwa dhulma, na kuendelea katika upotovu wao kwa kusema: Nyoyo zetu zimefungwa hazikubali hayo unayo tuitia! Nao hawasemi kweli katika kauli yao hiyo, bali Mwenyezi Mungu amezifuta nyoyo zao kwa ukafiri wao, basi ni wachache tu kati yao wanao amini.