۞ لَّا يُحِبُّ ٱللَّهُ ٱلۡجَهۡرَ بِٱلسُّوٓءِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ إِلَّا مَن ظُلِمَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعًا عَلِيمًا ١٤٨
Llā yuhibbullāhul-jahra bis-sū'i minal-qawli illā man zulima wakānallāhu samī'an 'alīmā
MWENYEZI MUNGU hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. 148
Maelezo ya chini
148 Mwenyezi Mungu anawakataza waja wake wasiseme maneno maovu, ila yule aliye patwa na dhulma. Ni halali kwake kumshitaki aliye mdhulumu, na autaje uovu aliyo tendewa. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mwenye kusikia vyema maneno ya aliye dhulumiwa. Na ni Mjuzi wa dhulma ya mwenye kudhulumu. Na atamlipa kwa kitendo chake hicho.