مَّا يَفۡعَلُ ٱللَّهُ بِعَذَابِكُمۡ إِن شَكَرۡتُمۡ وَءَامَنتُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ شَاكِرًا عَلِيمٗا ١٤٧
Mmā yaf'alullāhu bi'adhābikum in shakartum wa āmantum wakānallāhu shākiran 'alīmā
Mwenyezi Mungu hakuadhibuni mkimshukuru na mkamuamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea shukrani na ndiye Mwenye kujua. 147
Maelezo ya chini
147 Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hana alitakalo kwenu ila mumuamini Yeye, na muishukuru neema yake. Mkiwa hivyo basi hampati adhabu, bali mtapata malipo ya kheri na shukrani. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kushukuria waja wake kwa vitendo vyema, na ni Mjuzi, anajua hali zao zote njema na mbaya.