وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ ٤٣
Wamā arsalnā min qablika illā rijālan nūhī ilayhim fas'alū ahladh-dhikri in kuntum lā ta'lamūn
Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi(Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui. 43
Maelezo ya chini
43 Na kabla ya kukutuma wewe, ewe Nabii, kwa umma wako, hatukuwatuma kwa kaumu zilizo tangulia ila watu wanaume tulio wafunulia kwa Wahyi yale tunayo yataka wawafikishie. Wala hatukuwatuma Malaika kama watakavyo makafiri wa kaumu yako. Basi, enyi makafiri, waulizeni wenye kuvijua Vitabu vya mbinguni, kama nyinyi hamyajui hayo. Watajua kuwa Mitume wote wa Mwenyezi Mungu hawakuwa ila wanaadamu, wala si Malaika.