بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِۗ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلذِّكۡرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ ٤٤
Bil-bayyināti waz-zuburi wa anzalnā ilaykadh-dhikra litubayyina lin-nāsi mā nuzzila ilayhim wala'allahum yatafakkarūn
Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri. 44
Maelezo ya chini
44 Na hao Mitume tuliwaunga mkono kwa miujiza na dalili zilizo wazi za kuthibitisha ukweli wao. Na tuliwateremshia Vitabu vya kuwabainishia sharia zao zenye maslaha yao. Na wewe, ewe Nabii, tumekuteremshia Qur'ani uwabainishie watu Itikadi na Hikima ziliomo ndani yake, na uwatake waizingatie, kwa kutaraji kuwa watazingatia, na watawaidhika, na mambo yao yanyooke.