Surat An-Nahl, aya 42

16:42

ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ ٤٢

Alladhīna sabarū wa'alā rabbihim yatawakkalūn

Wale wanao subiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 42

Maelezo ya chini

42 Na hao Wahajiri (Walio hama) ndio walio vumilia adhabu walio ipata kwa sababu ya Itikadi yao, na wakamwachia hali yao Mwenyezi Mungu peke yake, bila ya kumbali mwenginewe. Kwa ajili ya hayo tumewapa bora ya malipo.