Surat An-Nahl, aya 102

16:102

قُلۡ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلۡقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلۡحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَهُدٗى وَبُشۡرَىٰ لِلۡمُسۡلِمِينَ ١٠٢

Qul nazzalahū rūhul-qudusi mir rabbika bil-haqqi liyuthabbital-ladhīna āmanū wahudan wabushrā lil-muslimīn

Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu. 102

Maelezo ya chini

102 Ewe Nabii! Waambie kuwabainishia muujiza wako: Hakika hii Qur'ani kaniteremshia mimi Jibril, Roho safi, kutokana kwa Mola wangu Mlezi, kwa kufuatana na kukusanya Haki, ili kwayo azitie imara nyoyo za Waumini, na ili iwe ni Uwongofu kwa watu wote waongokewe, na iwape bishara njema ya neema Waislamu wote.