وَإِذَا بَدَّلۡنَآ ءَايَةٗ مَّكَانَ ءَايَةٖ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مُفۡتَرِۭۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ ١٠١
Wa idhā baddalnā āyatam makāna āyatin wallāhu a'lamu bimā yunazzilu qālū innamā anta muftari bal aktharuhum lā ya'lamūn
Na tunapo badilisha Ishara pahala pa Ishara nyengine, na MwenyeziMungu anajua anayo teremsha, wao husema: Wewe ni mzushi. Bali wengi wao hawajui kitu. 101
Maelezo ya chini
101 Na tukikuletea muujiza badala ya muujiza ulio sawa na tulio waletea Manabii walio tangulia, na tukakuletea wewe hii Qur'ani kuwa ni muujiza wenyewe, wanakusingizia kuwa umeizua tu hii, na kwamba unamzulia Mwenyezi Mungu uwongo! Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mjuzi kwa ujuzi usio pikuliwa kuijua miujiza anayo wateremshia Manabii wake. Lakini wengi wao watu hawa si watu wa ilimu wa kujua lilio kweli.