Surat An-Nahl, aya 100

16:100

إِنَّمَا سُلۡطَٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوۡنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشۡرِكُونَ ١٠٠

Innamā sultānuhū 'alal-ladhīna yatawallawnahū walladhīna hum bihī mushrikūn

Hakika madaraka yake ni juu ya wanao mfanya rafiki yao, na wale wanao fanya ushirika naye. 100

Maelezo ya chini

100 Bali taathira yake Shetani na khatari yake ni juu ya wale ambao nyoyo zao hazina mfungamano wala mapenzi na Mwenyezi Mungu. Basi hao hawana la kuwalinda na athari za Shetani. Watamfuata huyo kama rafiki anavyo mfuata rafiki yake, mpaka watumbukie katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika kumuabudu pamoja na miungu mingine isiyo weza kuleta madhara wala manufaa.