Surat An-Nahl, aya 99

16:99

إِنَّهُۥ لَيۡسَ لَهُۥ سُلۡطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ ٩٩

Innahū laysa lahū sultānun 'alal-ladhīna āmanū wa'alā rabbihim yatawakkalūn

Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi. 99

Maelezo ya chini

99 Ukifanya haya kwa kumsafia niya Mwenyezi Mungu, basi atakulinda na Shetani, na atakuondolea wasiwasi. Kwani Shetani hana athari kwa walio jaa Imani ya Mwenyezi Mungu, na wakamtaka msaada na kumtegemea Yeye peke yake.