وَأَصۡبَحَ ٱلَّذِينَ تَمَنَّوۡاْ مَكَانَهُۥ بِٱلۡأَمۡسِ يَقُولُونَ وَيۡكَأَنَّ ٱللَّهَ يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ وَيَقۡدِرُۖ لَوۡلَآ أَن مَّنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡنَا لَخَسَفَ بِنَاۖ وَيۡكَأَنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلۡكَٰفِرُونَ ٨٢
Wa asbahal-ladhīna tamannaw makānahū bil-amsi yaqūlūna wayka'annallāha yabsutur-rizqa liman yashā'u min 'ibādihī wayaqdiru lawlā am mannallāhu 'alaynā lakhasafa binā wayka'annahū lā yuflihul-kāfirūn
Na wale walio tamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema: Kumbe Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humdhikisha amtakaye. Ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani angeli tudidimiza. Kumbe makafiri hawafanikiwi! 82
Maelezo ya chini
82 Na wale walio kuwa karibuni wakikitamani cheo chake cha duniani, wakawa wanatamka maneno ya masikitiko na majuto baada ya kuyafikiri yaliyo msibu yeye. Wakawa wanasema: Hakika Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake Waumini na wasio kuwa Waumini. Na humdhikisha amtakaye katika hao. Na wakawa wanasema kwa kushukuru: Lau kuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani kwa kutupa uwongofu tukafuata Imani, na akatuhifadhi tusiporonyoke angeli tutia katika mitihani kwa kutukubalia tuliyo kuwa tunayatamani, na akatufanyia kama alivyo mfanyia Qaruni. Hakika wanao ipinga neema ya Mwenyezi Mungu hawafanikiwi kwa kuokoka na adhabu yake.