تِلۡكَ ٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ نَجۡعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوّٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فَسَادٗاۚ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ ٨٣
Tilkad-dārul-ākhiratu naj'aluhā lilladhīna lā yurīdūna 'uluwwan fil-ardi walā fasādan wal-'āqibatu lil-muttaqīn
Hayo ndiyo makaazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasio taka kujitukuza duniani wala ufisadi. Na mwisho mwema ni wa wachamngu. 83
Maelezo ya chini
83 Hayo ndio makaazi ambayo umesikia khabari zake, ewe Mtume, na zikakufikia sifa zake, nayo ni Pepo. Tumeiweka makhsusi kwa ajili ya Waumini wat'iifu, wasio taka kujipa ubora na utukufu wa kidunia, na wala hawapotoki kuendea ufisadi na maasi. Na mwisho mwema ni wa wale ambao nyoyo zao zimejaa khofu ya Mwenyezi Mungu, na wanatenda yanayo mridhisha Yeye.