Surat Al-Qasas, aya 81

28:81

فَخَسَفۡنَا بِهِۦ وَبِدَارِهِ ٱلۡأَرۡضَ فَمَا كَانَ لَهُۥ مِن فِئَةٖ يَنصُرُونَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُنتَصِرِينَ ٨١

Fakhasafnā bihī wabidārihil-arda famā kāna lahū min fi atin yansurūnahū min dūnillāhi wamā kāna minal-muntasirīn

Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanao jitetea. 81

Maelezo ya chini

81 Mwenyezi Mungu akamdidimiza katika ardhi, na ardhi ikammeza yeye na nyumba yake na vyote vilio kuwemo ndani yake, mali na mapambo yake. Hakuwa na wasaidizi wa kumkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wala yeye mwenyewe hakuweza kujinusuru nafsi yake.