Surat Al-Ma'idah, aya 75

5:75

مَّا ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ إِلَّا رَسُولٞ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِهِ ٱلرُّسُلُ وَأُمُّهُۥ صِدِّيقَةٞۖ كَانَا يَأۡكُلَانِ ٱلطَّعَامَۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ ٱنظُرۡ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ ٧٥

Mmal-masīhubnu maryama illā rasūlun qad khalat min qablihir-rusulu wa ummuhū siddīqatun kānā ya'kulānit-ta'āmanzur kayfa nubayyinu lahumul-āyāti thummanzur annā yu'fakūn

Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyo wabainishia Aya, kisha angalia vipi wanavyo geuzwa. 75

Maelezo ya chini

75 Isa bin Maryamu si chochote ila ni mwanaadamu aliye pata neema ya Mwenyezi Mungu kwa kuteuliwa kuwa ni Mtume kama walivyo mtangulia wengi kabla yake. Na Mama yake Isa ni mmoja katika wanawake, aliye jaaliwa kuwa ni mkweli katika kauli yake na mwenye kumuamini Mola wake Mlezi. Na yeye na mwanawe, Isa, walikuwa wana mahitajio yanayo hitajiwa na kila mwanaadamu, kama kula na kunywa, na kwenda haja. Na hizo ni dalili za ubinaadamu wao. Basi hebu zingatia, ewe mwenye kusikia, hali ya hao walio ingia upofu hata hawaoni dalili za Ishara zilizo wazi ambazo amewabainishia Mwenyezi Mungu. Tena zingatia vipi wanaiacha Haki juu ya kuwa ni iwazi kabisa.