أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى ٱللَّهِ وَيَسۡتَغۡفِرُونَهُۥۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ٧٤
Afalā yatūbūna ilallāhi wayastaghfirūnahū wallāhu ghafūrur rahīm
Je! Hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. 74
Maelezo ya chini
74 Je! Watu hawa hawaziachilii mbali hizo itikadi za uzushi na uwongo, wakarejea kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu, na wakaomba wafutiwe dhambi zao walizo zitenda? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa maghfira, Mwingi wa rehema.