Surat Al-Ma'idah, aya 76

5:76

قُلۡ أَتَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمۡلِكُ لَكُمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗاۚ وَٱللَّهُ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ٧٦

Qul ata'budūna min dūnillāhi mā lā yamliku lakum darran walā naf'an wallāhu huwas-samī'ul-'alīm

Sema: Je! Mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukufaeni? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua. 76

Maelezo ya chini

76 Ewe Mtume! Waambie hawa wapotovu: Vipi mnamuabudu mungu asiye weza kukudhuruni kwa lolote mkiacha kumuabudu, wala hawezi kukufaeni kwa lolote mkimuabudu!! Vipi mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu ambaye Yeye ndiye Mungu Mwenye uweza wa kila kitu, naye ni Mwenye kusikia, na Mwenye ujuzi.