Surat Al-Ma'idah, aya 56

5:56

وَمَن يَتَوَلَّ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَإِنَّ حِزۡبَ ٱللَّهِ هُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ ٥٦

Waman yatawallallāha warasūlahū walladhīna āmanū fa inna hizballāhi humul-ghālibūn

Na atakaye fanya urafiki na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, basi hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda. 56

Maelezo ya chini

56 Na mwenye kufanya urafiki na Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini na wakawa hao ndio wa kuwategemea kwa msaada na nusura, basi huyo atakuwa katika Hizbu (yaani kundi) ya Mwenyezi Mungu, na Hizbu ya Mwenyezi Mungu ndio yenye kushinda na kufuzu.