إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُمۡ رَٰكِعُونَ ٥٥
Innamā waliyyukumullāhu warasūluhū walladhīna āmanul-ladhīna yuqīmūnas-salawāta wayu'tūnaz-zakawāta wahum rāki'ūn
Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na walio amini, ambao hushika Sala na hutoa Zaka nao wananyenyekea. 55
Maelezo ya chini
55 Enyi Waumini! Urafiki wenu nyinyi uwe na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na nyinyi kwa nyinyi katika wanao shika Swala, na wanatoa Zaka, nao wananyenyekea.