يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَكُمۡ هُزُوٗا وَلَعِبٗا مِّنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَٱلۡكُفَّارَ أَوۡلِيَآءَۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ٥٧
Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū lā tattakhidhul-ladhīnat-takhadhū dīnakum huzuwan wala'ibam minal-ladhīna ūtul-kitāba min qablikum wal-kuffāra awliyā'a wattaqullāha in kuntum mu'minīn
Enyi mlio amini! Msiwafanye marafiki wale walio ifanyia kejeli na mchezo Dini yenu miongoni mwa walio pewa Kitabu kabla yenu, na makafiri wengine. Na mcheni Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wenye kuamini. 57
Maelezo ya chini
57 Enyi mlio amini! Msiwafanye maadui wa Uislamu walio ifanyia maskhara Dini yenu wakaichezea - nao ni Mayahudi na Wakristo na washirikina, kuwa ndio wasaidizi, wala msifanye urafiki nao. Na mkhofuni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wakweli katika Imani yenu.