فَتَرَى ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ يُسَٰرِعُونَ فِيهِمۡ يَقُولُونَ نَخۡشَىٰٓ أَن تُصِيبَنَا دَآئِرَةٞۚ فَعَسَى ٱللَّهُ أَن يَأۡتِيَ بِٱلۡفَتۡحِ أَوۡ أَمۡرٖ مِّنۡ عِندِهِۦ فَيُصۡبِحُواْ عَلَىٰ مَآ أَسَرُّواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ نَٰدِمِينَ ٥٢
Fataral-ladhīna fī qulūbihim maradun yusāri'ūna fīhim yaqūlūna nakhshā an tusībanā dā'iratun fa'asallāhu an ya'tiya bil-fathi aw amrim min 'indihī fayusbihū 'alā mā asarrū fī anfusihim nādimīn
Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jingine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao. 52
Maelezo ya chini
52 Ilivyo kuwa kuwafanya hao marafiki hawafanyi ila walio dhulumu, basi utaona kuwa wanao wafanya makafiri ndio rafiki zao wana maradhi katika nyoyo zao, maradhi ya udhoofu na unaafiki. Wao husema: Tunaogopa usije kutupata msiba kwa kugeuka mambo na wao wasitusaidie! A'saa, huenda, Mwenyezi Mungu akamletea Mtume wake kufunguka mambo, na Waislamu wakawashinda maadui zao, au ukadhihiri unaafiki wa hao wanaafiki, wakaamkia majuto, wakijuta kwa zile kufuru na shaka shaka walizo kuwa wakizificha katika nafsi zao.