Surat Al-Ma'idah, aya 53

5:53

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَهَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ إِنَّهُمۡ لَمَعَكُمۡۚ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡ فَأَصۡبَحُواْ خَٰسِرِينَ ٥٣

Wayaqūlul-ladhīna āmanū ahā'ulā'il-ladhīna aqsamū billāhi jahda aymānihim innahum lama'akum habitat a'māluhum fa asbahū khāsirīn

Na walio amini watasema: Hivyo hawa ndio wale walio apa ukomo wa viapo vyao kuwa wao wa pamoja nanyi? Vitendo vyao vitapotea bure, na wataamkia kuwa wenye kukhasirika. 53

Maelezo ya chini

53 Na hapo tena Waumini wa kweli watasema kuwastaajabia wanaafiki: Ndio hawa walio kula yamini kwa viapo vya kupita kiasi kwa jina la Mwenyezi Mungu, ya kwamba wao ni wenzenu katika Dini, wenye kuamini kama nyinyi? Wamesema uwongo! Na vitendo vyao vimefisidika, wakawa wamekosa Imani na nusura kutokana na Waumini.