وَلۡيَحۡكُمۡ أَهۡلُ ٱلۡإِنجِيلِ بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فِيهِۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡفَٰسِقُونَ ٤٧
Walyahkum ahlul-injīli bimā anzalallāhu fīhi wamal lam yahkum bimā anzalallāhu fa ulā'ika humul-fāsiqūn
Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu. 47
Maelezo ya chini
47 Na Sisi tuliwaamrisha wafuasi wa Isa, yaani Watu wa Injili, Wakristo, wahukumu kwa hukumu alizo teremsha Mwenyezi Mungu. Na wasio hukumu kwa mujibu wa alivyo teremsha Mwenyezi Mungu basi hao wameiacha Sharia ya Mwenyezi Mungu, ni waasi.