وَكَيۡفَ يُحَكِّمُونَكَ وَعِندَهُمُ ٱلتَّوۡرَىٰةُ فِيهَا حُكۡمُ ٱللَّهِ ثُمَّ يَتَوَلَّوۡنَ مِنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٤٣
Wakayfa yuhakkimūnaka wa'indahumut-tawrātu fīhā hukmullāhi thumma yatawallawna mim ba'di dhālika wamā ulā'ika bil-mu'minīn
Na huwaje wakufanye wewe hakimu nao wanayo Taurati yenye hukumu za Mwenyezi Mungu? Kisha baada ya hayo wanageuka. Na hao si wenye kuamini. 43
Maelezo ya chini
43 Ama ajabu ya watu hawa Mayahudi! Vipi wanataka hukumu yako na hali wao wanayo hukumu ya Mwenyezi Mungu imeandikwa katika Taurati? Na kinacho staajabisha ni kuwa wao huikataa hukumu yako inapo kuwa haikubaliani na mapendeleo yao, ijapo kuwa imewafikiana na ilivyo katika kitabu chao! Watu hawa sio miongoni mwa Waumini wanaoit'ii Haki.