إِنَّآ أَنزَلۡنَا ٱلتَّوۡرَىٰةَ فِيهَا هُدٗى وَنُورٞۚ يَحۡكُمُ بِهَا ٱلنَّبِيُّونَ ٱلَّذِينَ أَسۡلَمُواْ لِلَّذِينَ هَادُواْ وَٱلرَّبَّٰنِيُّونَ وَٱلۡأَحۡبَارُ بِمَا ٱسۡتُحۡفِظُواْ مِن كِتَٰبِ ٱللَّهِ وَكَانُواْ عَلَيۡهِ شُهَدَآءَۚ فَلَا تَخۡشَوُاْ ٱلنَّاسَ وَٱخۡشَوۡنِ وَلَا تَشۡتَرُواْ بِـَٔايَٰتِي ثَمَنٗا قَلِيلٗاۚ وَمَن لَّمۡ يَحۡكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ ٤٤
Innā anzalnat-tawrāta fīhā hudan wanūrun yahkumu bihan-nabiyyūnal-ladhīna aslamū lilladhīna hādū war-rabbāniyyūna wal-ahbāru bimastuhfizū min kitābillāhi wakānū 'alayhi shuhadā'a falā takhshawun-nāsa wakhshawni walā tashtarū bi'āyātī thamanan qalīlan wamal lam yahkum bimā anzalallāhu fa ulā'ika humul-kāfirūn
Hakika Sisi tuliteremsha Taurati yenye uwongofu na nuru, ambayo kwayo Manabii walio nyenyekea kiislamu, na wachamngu, na wanazuoni, waliwahukumu Mayahudi; kwani walikabidhiwa kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Nao wakawa ni mashahidi juu yake. Basi msiwaogope watu, bali niogopeni Mimi. Wala msibadilishe Aya zangu kwa thamani chache. Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri. 44
Maelezo ya chini
44 Hakika Sisi tumemteremshia Musa Taurati. Ndani yake mna uwongofu unao endea Haki, na mna bayana yenye kutoa mwangaza unao nawirisha hukumu wanazo zihukumia Manabii, na wale walio safisha nafsi zao kwa ajili ya Mola wao Mlezi, na wanazuoni wenye kufwata njia ya Manabii, na wale walio chukua ahadi kukihifadhi Kitabu cha Mwenyezi Mungu kisibadilishwe, kwa kukilinda na kushuhudia kuwa hicho ndiyo Haki. Basi msiwakhofu watu mnapo hukumu, na nikhofuni Mimi tu, Mimi Mola wenu Mlezi, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Wala msizibadilishe Aya zangu nilizo ziteremsha kwa thamani duni ya kutaka starehe ya dunia, kama vile mrungura au kutaka cheo! Na wote wasio hukumu kwa mujibu alivyo teremsha Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa makafiri.