Surat Al-Ma'idah, aya 119

5:119

قَالَ ٱللَّهُ هَٰذَا يَوۡمُ يَنفَعُ ٱلصَّٰدِقِينَ صِدۡقُهُمۡۚ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ رَّضِيَ ٱللَّهُ عَنۡهُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ١١٩

Qālallāhu hādhā yawmu yanfa'us-sādiqīna sidquhum lahum jannātun tajrī min tahtihal-anhāru khālidīna fīhā abadar radiyallāhu 'anhum waradū 'anhu dhālikal-fawzul-'azīm

Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa. 119

Maelezo ya chini

119 Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Watapata mabustani yanayo pitiwa na mito chini ya miti yake. Na humo watakaa, wala hawatatoka milele, wakistarehe humo kwa radhi ya Mwenyezi Mungu anavyo waridhia wao, na wao watavyo kuwa radhi kwa malipo alio walipa. Na Neema hiyo ndio kufuzu kukubwa.