Surat Al-Ma'idah, aya 118

5:118

إِن تُعَذِّبۡهُمۡ فَإِنَّهُمۡ عِبَادُكَۖ وَإِن تَغۡفِرۡ لَهُمۡ فَإِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ ١١٨

In tu'addhibhum fa innahum 'ibāduka wa in taghfir lahum fa innaka antal-'azīzul-hakīm

Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. 118

Maelezo ya chini

118 Ukiwaadhibu kwa waliyo yatenda basi hao ni waja wako, unawafanya upendavyo. Na ukiwasamehe, basi hakika Wewe peke yako ndiye Mtenda nguvu usiye shindwa, Mwenye hikima yenye kufikilia kila linalo toka kwako.