وَإِذۡ أَوۡحَيۡتُ إِلَى ٱلۡحَوَارِيِّـۧنَ أَنۡ ءَامِنُواْ بِي وَبِرَسُولِي قَالُوٓاْ ءَامَنَّا وَٱشۡهَدۡ بِأَنَّنَا مُسۡلِمُونَ ١١١
Wa idh awhaytu ilal-hawāriyyina an āminū bī wabirasūlī qālū āmannā washhad bi annanā muslimūn
Na nilipo wafunulia Wanafunzi kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema: Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu. 111
Maelezo ya chini
111 Ewe Mtume! Watajie umma wako yaliyo tokea tulipo watia hima kikundi cha alio wataka Isa wamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake Isa, na wakamuitikia wakawa ndio Wanafunzi wake makhsusi, na wakasema: Tumeamini. Na shuhudia ewe Mola wetu Mlezi, kuwa sisi tumesafi niya zetu, na tunafuata amri zako, yaani Waislamu.