Surat Al-Ma'idah, aya 112

5:112

إِذۡ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ هَلۡ يَسۡتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيۡنَا مَآئِدَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِۖ قَالَ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ١١٢

Idh qālal-hawāriyyūna yā'īsabna maryama hal yastatī'u rabbuka an yunazzila 'alaynā mā'idatam minas-samā'i qālat-taqullāha in kuntum mu'minīn

Wanafunzi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Je, Mola wako Mlezi anaweza kututeremshia chakula kutoka mbinguni? Akasema: Mcheni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini. 112

Maelezo ya chini

112 Ewe Nabii! Taja pia yaliyo tokea pale wafuasi wa Isa wenye ikhlasi walipo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Hivyo Mola wako Mlezi atakuitikia ukimtaka akuteremshie chakula kutoka mbinguni? Isa akawaambia kuwajibu: Kama nyinyi ni kweli mnamuamini Mwenyezi Mungu, basi mkhofuni Yeye, na fuateni amri zake na makatazo yake. Wala msitafute hoja ila nilizo kuleteeni.