Surat Al-Kahf, aya 86

18:86

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَغۡرِبَ ٱلشَّمۡسِ وَجَدَهَا تَغۡرُبُ فِي عَيۡنٍ حَمِئَةٖ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوۡمٗاۖ قُلۡنَا يَٰذَا ٱلۡقَرۡنَيۡنِ إِمَّآ أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّآ أَن تَتَّخِذَ فِيهِمۡ حُسۡنٗا ٨٦

Hattā idhā balagha maghribash-shamsi wajadahā taghrubu fī 'aynin hami'atin wawajada 'indahā qawman qulnā yādhal-qarnayni immā an tu'addhiba wa immā an tattakhidha fīhim husnā

Hata alipo fika machwea-jua aliliona linatua katika checmchem yenye matope meusi. Na hapo akawakuta watu. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Ama uwaadhibu au watwae kwa wema. 86

Maelezo ya chini

86 Akenda mpaka akafika pahala mbali huko upande wa magharibi, akalikuta jua kwa linavyo onekana kwa macho kama kwamba linazama pahala penye chemchem ya maji ya moto na matope meusi. Na karibu ya chemchem hii Dhul- Qarnaini aliwakuta watu makafiri. Mwenyezi Mungu akamtia moyoni mwake afanye mojapo ya mambo mawili: Ama awaite kwenye Imani, na hili kwa hakika ni jambo zuri; au awapige vita ikiwa hawakuitikia wito wa Imani.