Surat Al-Kahf, aya 71

18:71

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا رَكِبَا فِي ٱلسَّفِينَةِ خَرَقَهَاۖ قَالَ أَخَرَقۡتَهَا لِتُغۡرِقَ أَهۡلَهَا لَقَدۡ جِئۡتَ شَيۡـًٔا إِمۡرٗا ٧١

Fantalaqā hattā idhā rakibā fis-safīnati kharaqahā qāla akharaqtahā litughriqa ahlahā laqad ji'ta shay'an imrā

Basi wawili hao wakatoka, hata walipo panda jahazi (yule mtu) akaitoboa. (Musa) akasema: Unaitoboa uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya. 71

Maelezo ya chini

71 Wakatoka wakitambaa na mfukwe wa bahari mpaka wakakuta jahazi wakaipanda. Yule mja mwema akaitoboa jahazi ile nayo imo safarini. Musa akapinga kwa kusema: Umeitoboa makusudi upate kuwazamisha watu wake? Ama hakika umefanya jambo ovu!