Surat Al-Kahf, aya 50

18:50

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ كَانَ مِنَ ٱلۡجِنِّ فَفَسَقَ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِۦٓۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّيَّتَهُۥٓ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِي وَهُمۡ لَكُمۡ عَدُوُّۢۚ بِئۡسَ لِلظَّٰلِمِينَ بَدَلٗا ٥٠

Wa idh qulnā lil-malā'ikatisjudū li'ādama fasajadū illā iblīsa kāna minal-jinni fafasaqa 'an amri rabbihī afatattakhidhūnahū wadhurriyyatahū awliyā'a min dūnī wahum lakum 'aduwwu bi sa liz-zālimīna badalā

Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu. 50

Maelezo ya chini

50 Ewe Mtume! Watajie mwanzo wa kuumbwa kwao, ili wajue kuwa wao wametokana na udongo, basi wasikae wakidanganyika na hayo waliyo nayo, wakamnyenyekea Iblisi, adui wa baba yao. Kwani yeye alikuwa katika majini, akajivuna, na akamuasi Mwenyezi Mungu. Basi yawaje baada ya kwisha jua khabari zake mkamfanya yeye na kizazi chake kuwa ndio wasaidizi wenu badala ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio adui zenu! Badala hii ni ovu kwa mwenye kuidhulumu nafsi yake na akamt'ii Shetani.