Surat Al-Isra, aya 37

17:37

وَلَا تَمۡشِ فِي ٱلۡأَرۡضِ مَرَحًاۖ إِنَّكَ لَن تَخۡرِقَ ٱلۡأَرۡضَ وَلَن تَبۡلُغَ ٱلۡجِبَالَ طُولٗا ٣٧

Walā tamshi fil-ardi marahan innaka lan takhriqal-arda walan tablughal-jibāla tūlā

Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima. 37

Maelezo ya chini

37 Wala usitembee katika ardhi kwa kiburi na majivuno. Kwani vyovyote utavyo fanya huwezi kuipasua ardhi kwa nguvu za mkanyago wako, na kama utavyo kuwa mrefu huwezi kuipita urefu milima.