Surat Al-Isra, aya 36

17:36

وَلَا تَقۡفُ مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٌۚ إِنَّ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡبَصَرَ وَٱلۡفُؤَادَ كُلُّ أُوْلَٰٓئِكَ كَانَ عَنۡهُ مَسۡـُٔولٗا ٣٦

Walā taqfu mā laysa laka bihī 'ilmun innas-sam'a wal-basara wal-fu'āda kullu ulā'ika kāna 'anhu mas'ūlā

Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo vyote vitasailiwa. 36

Maelezo ya chini

36 Ewe mtu! Usifuate maneno wala vitendo usivyo vijua. Basi usiseme: Nimesikia...na hali hukusikia. Au: Najua...na hali hujui. Kwani masikio, macho na moyo, vyote hivyo Siku ya Kiyama vitamuuliza mtu kwa alivyo tenda kwavyo.