Surat Al-Isra, aya 32

17:32

وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓۖ إِنَّهُۥ كَانَ فَٰحِشَةٗ وَسَآءَ سَبِيلٗا ٣٢

Walā taqrabuz-zinā innahū kāna fāhishatan wasā'a sabīlā

Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya. 32

Maelezo ya chini

32 Wala msiukaribie uzinzi, kwa kuziingilia sababu zinazo pelekea uzinzi. Jambo hilo ni jambo la aibu na uovu usio fichikana, na hapana njia mbovu kama hiyo.