Surat Al-Imran, aya 79

3:79

مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤۡتِيَهُ ٱللَّهُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُواْ عِبَادٗا لِّي مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَٰكِن كُونُواْ رَبَّٰنِيِّـۧنَ بِمَا كُنتُمۡ تُعَلِّمُونَ ٱلۡكِتَٰبَ وَبِمَا كُنتُمۡ تَدۡرُسُونَ ٧٩

Mā kāna libasharin an yu'tiyahullāhul-kitāba wal-hukma wan-nubuwwata thumma yaqūla lin-nāsi kūnū 'ibādal lī min dūnillāhi walākin kūnū rabbāniyyina bimā kuntum tu'allimūnal-kitāba wabimā kuntum tadrusūn

Haiwezi kuwa mtu aliye pewa na Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima na Unabii kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu. Bali atawaambia: Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma. 79

Maelezo ya chini

79 Si akili wala haimfalii mwanaadamu aliye teremshiwa Kitabu na Mwenyezi Mungu na akapewa ilimu ya manufaa na kuweza kuzungumza mambo yanayo tokana na Mwenyezi Mungu, tena awatake watu wamuabudu yeye badala ya kumuabudu Mwenyezi Mungu. Lakini linalo ingia akilini, na lifaalo, ni kuwa yeye awatake watu wamsafie ibada Mola wao Mlezi aliye waumba kwa mujibu alivyo wafunza kutokana na ilimu ya Kitabu na kwa mujibu ya wanayo soma.