وَلَا يَأۡمُرَكُمۡ أَن تَتَّخِذُواْ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ أَرۡبَابًاۚ أَيَأۡمُرُكُم بِٱلۡكُفۡرِ بَعۡدَ إِذۡ أَنتُم مُّسۡلِمُونَ ٨٠
Walā ya'murakum an tattakhidhul-malā'ikata wan-nabiyyina arbāban aya'murukum bil-kufri ba'da idh antum muslimūn
Wala hatakuamrisheni kuwafanya Malaika na Manabii kuwa ni miungu. Je, atakuamrisheni ukafiri baada ya kuwa nyinyi Waislamu? 80
Maelezo ya chini
80 Wala hayumkini akuamrisheni kuwafanya Malaika au Manabii kuwa ndio miungu badala ya Mwenyezi Mungu. Ni ukafiri usio ingia akilini kukuamrisheni hayo baada ya kuwa mmekwisha kuwa Waislamu mlio muelekezea nyuso Mwenyezi Mungu. (Nabii Isa a.s. hakujidaia Ungu hata katika Injili hizi zilizo korogwa, wala hakumfanya Roho Mtakatifu, ambaye ni Malaika, kuwa ni Mungu.)