وَإِنَّ مِنۡهُمۡ لَفَرِيقٗا يَلۡوُۥنَ أَلۡسِنَتَهُم بِٱلۡكِتَٰبِ لِتَحۡسَبُوهُ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَمَا هُوَ مِنَ ٱلۡكِتَٰبِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ وَمَا هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ وَيَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ ٧٨
Wa inna minhum lafarīqan yalwūna alsinatahum bil-kitābi litahsabūhu minal-kitābi wamā huwa minal-kitābi wayaqūlūna huwa min 'indillāhi wamā huwa min 'indillāhi wayaqūlūna 'alallāhil-kadhiba wahum ya'lamūn
Na wapo baadhi yao wanao pindua ndimi zao katika kusoma Kitabu ili mdhanie kuwa hayo yanatoka Kitabuni, na wala hayatoki Kitabuni. Na husema: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na wala hayatoki kwa Mwenyezi Mungu. Na wanamsingizia Mwenyezi Mungu uwongo na wao wanajua. 78
Maelezo ya chini
78 Katika Watu wa Kitabu wapo ambao huzipindua ndimi zao kutamka maneno yasiyo kuwamo katika Kitabu kwa lafdhi ya Kitabu, watu wadhanie kuwa ni maneno yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, na wala hayamo katika ufunuo wa Mwenyezi Mungu. Wanamzulia Mwenyezi Mungu nao ndani ya nafsi zao wanajua kuwa wanasema uwongo.