إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ ٱلَّذِي جَعَلۡنَٰهُ لِلنَّاسِ سَوَآءً ٱلۡعَٰكِفُ فِيهِ وَٱلۡبَادِۚ وَمَن يُرِدۡ فِيهِ بِإِلۡحَادِۭ بِظُلۡمٖ نُّذِقۡهُ مِنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ ٢٥
Innal-ladhīna kafarū wayasuddūna 'an sabīlillāhi wal-masjidil-harāmil-ladhī ja'alnāhu lin-nāsi sawā'anil-'ākifu fīhi wal-bādi waman yurid fīhi bi ilhādi bizulmin nudhiqhu min 'adhābin alīm
Hakika wale walio kufuru na wakazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu na Msikiti Mtakatifu, ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni. Na kila atakaye taka kufanya upotofu humo kwa dhulma, basi tutamwonjesha adhabu chungu. 25
Maelezo ya chini
25 Hakika wale walio kufuru, yaani walio mkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na pamoja na hayo wakawa mtindo wao kuwazuia watu wasiingie katika Uislamu, na kuwafanyia pingamizi Waumini kuingia kwenye Msikiti Mtakatifu wa Makka - na ilhali Mwenyezi Mungu ameufanya huo ni pahala pa amani kwa watu wote, mkaazi na mpita njia - atawapa watu hao adhabu kali. Na hali kadhaalika kila atakaye kengeuka na Haki, na akatenda udhalimu wowote katika pahala patakatifu, Mwenyezi Mungu atamuadhibu adhabu ya kutia uchungu.