Surat Al-Hajj, aya 15

22:15

مَن كَانَ يَظُنُّ أَن لَّن يَنصُرَهُ ٱللَّهُ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ فَلۡيَمۡدُدۡ بِسَبَبٍ إِلَى ٱلسَّمَآءِ ثُمَّ لۡيَقۡطَعۡ فَلۡيَنظُرۡ هَلۡ يُذۡهِبَنَّ كَيۡدُهُۥ مَا يَغِيظُ ١٥

Man kāna yazunnu al lan yansurahullāhu fid-dunyā wal-ākhirati falyamdud bisababin ilas-samā'i thumma lyaqta' falyanzur hal yudhhibanna kayduhū mā yaghīz

Anaye dhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru (Mtume) katika dunia na Akhera na afunge kamba kwenye dari kisha aikate. Atazame je hila yake itaondoa hayo yaliyo mkasirisha? 15

Maelezo ya chini

15 Ikiwa miongoni mwa makafiri yupo anaye dhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamsaidia Nabii wake, basi na anyooshe kamba mpaka kwenye dari ya nyumba yake. Kisha ajinyonge, na akadirie katika nafsi yake na atazame, je, kitendo chake hicho kitaondoa hayo yanayo muudhi ya kuwa Mwenyezi Mungu anamnusuru Mtume wake?