إِنَّ ٱللَّهَ يُدۡخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَفۡعَلُ مَا يُرِيدُ ١٤
Innallāha yudkhilul-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti jannātin tajrī min tahtihal-anhāru innallāha yaf'alu mā yurīd
Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitazo mito kati yake. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakayo. 14
Maelezo ya chini
14 Hakika wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake kwa Imani yenye kuambatana na vitendo vyema, Mola wao Mlezi atawatia Siku ya Kiyama katika Bustani zipitwazo chini ya miti yake na mito. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda apendavyo kumuadhibu mharibifu na kumlipa mema mtenda mema.