وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُكُمۡ أَن تَذۡبَحُواْ بَقَرَةٗۖ قَالُوٓاْ أَتَتَّخِذُنَا هُزُوٗاۖ قَالَ أَعُوذُ بِٱللَّهِ أَنۡ أَكُونَ مِنَ ٱلۡجَٰهِلِينَ ٦٧
Wa idh qāla mūsā liqawmihī innallāha ya'murukum an tadhbahū baqaratan qālū atattakhidhunā huzuwan qāla a'ūdhu billāhi an akūna minal-jāhilīn
Na Musa alipo waambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje Ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: Audhubil lahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga. 67
Maelezo ya chini
67 Na kumbukeni pale alipo uliwa mtu na asijuulikane muuwaji, Musa akawaambia watu wake: Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje Ng'ombe ili iwe ndio ufunguo wa kumgundua muuwaji. Lakini wakaona hayo ni mageni, baina ya yale mauwaji na kumchinja ng'ombe. Wakasema: Unatufanyia maskhara wewe Musa? Yeye akawajibu: Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu asinipatilize kwa kuwa katika wajinga wanao wadhihaki waja wake.