قَالُواْ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ يُبَيِّن لَّنَا مَا هِيَۚ قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٞ لَّا فَارِضٞ وَلَا بِكۡرٌ عَوَانُۢ بَيۡنَ ذَٰلِكَۖ فَٱفۡعَلُواْ مَا تُؤۡمَرُونَ ٦٨
Qālud'u lanā rabbaka yubayyil lanā mā hiya qāla innahū yaqūlu innahā baqaratul lā fāridun walā bikrun 'awānu bayna dhālika faf'alū mā tu'marūn
Wakasema: Tuombee kwa Mola wako Mlezi atupambanulie ni Ng'ombe gani? Akasema: Hakika Yeye anasema kwamba Ng'ombe huyo si mpevu, wala si kinda, bali ni wa katikati baina ya hao. Basi fanyeni mnavyo amrishwa. 68
Maelezo ya chini
68 Tena wakamwambia Musa wakirejea lile shauri la ng'ombe: Tutakie kwa Mola wako Mlezi atubainishie sifa za huyo ng'ombe. Akawaambia: Mwenyezi Mungu ameniambia huyo Ng'ombe si mkubwa wala si mdogo, bali yu katikati baina ya upevu na uchanga. Basi hebu tekelezeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu